Home » » Ndugu wamtelekeza mgonjwa kituo cha basi kukwepa gharama hospitalini

Ndugu wamtelekeza mgonjwa kituo cha basi kukwepa gharama hospitalini


 Beda Mapengo (40), makazi  wa  kijiji  cha  Majomoto  katika mkoa  wa Katavi  juzi  akisaidiwa  kutolewa kwenye  basi  la Mbeya Express  T844 ARZ  na  wapiga  debe na  mawakala  katika Kituo  Kiuu  cha mabasi  mjini Sumbawanga mara baada ya kusafirishwa  kutoka Mbeya hadi mjini hapa, baada ya  kutelekezwa kituoni  hapo na  ndugu  zake kutokana na  kushindwa kumuhudumia  katika Hospitali ya Rufaa  mjini  humo ambako  alilazwa  zaidi  ya mwaka na nusu   baada ya  kuooza kiwili  wili  kufuatia   ajali  ya  gari. Picha na Mussa Mwangoka.

Beda Mapengo (40),makazi  wa  kijiji  cha  Majomoto  katika mkoa  wa Katavi  akiwa amelezwa katika Hospitali  ya Mkoa  wa Rukwa mjini  Sumbawanga  jana  baada ya kutelekezwa  na  ndugu  zake  katika Stendi kuu  ya mabasi  mjini   Mbeya  baada ya kushindwa kumuhudumia  katika Hospitali ya Rufaa  mjini  humo ambako  alikolazwa  zaidi  ya mwaka na nusu   baada ya  kupooza kiwiliwili  kufuatia   ajali  ya  gari. Picha na Mussa Mwangoka.


******************
Mussa Mwangoka, Sumbawanga. Rukwa yetu 

Mkazi  mmoja wa kijiji  cha Majimoto  Wilayani  Mlele, Mkoa  wa  Katavi, Beda Mapengo (40)  amedai kutoroshwa hospitalini na ndugu zake kumtelekeza katika kituo cha mabasi cha Mbeya mjini kwa madai  kuwa  hawana uwezo  wa  kifedha  wa  kuendelea  kumuuguza ugonjwa wake alioupata baada ya kugongwa na gari.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana katika hospitali ya Mkoa mjini Sumbawanga ambako amelazwa katika wodi namba tatu Mapengo alisema kuwa awali alilazwa kwa  zaidi  ya  mwaka  mmoja na nusu katika  Hospitali  ya Rufaa  Mkoani  Mbeya.

Hadi  juzi  alipochukuliwa na  ndugu  zake  ambao  hakuwa  tayari  kuwataja  majina  yao  na kumtorosha  hospitalini hapo kisha kumtelekeza  bila  msaada  wowote katika  Kituo  Kikuu  cha  mabasi   mjini  Mbeya.

Mapengo ambaye ni baba  mzazi  wa  watoto  wanne  aligongwa na gari wakati akitembea kwa miguu mwaka mmoja na nusu uliopita kijijini  Majimoto na sasa hawezi kukaa wala kutembea  kutokana  na  kiwiliwili  na  miguu  yake  kupooza.

“ Mie mwenyewe nimeshachoka  kuendelea  kuishi  hospitalini  sasa  ninachohitaji  ni  kupewa  msaada  ili   niweze  kurejeshwa kijijini  kwangu  Majimoto  kwani  hata  ndugu  zangu  hawana  tena   uwezo  wa  kunihudumia  kifedha kwani  wameniachia  sh.10,00 za  kujikimu” alisema

Kufuatia  kadhia hiyo yakutelekezwa na  ndugu  zake  hapo  Kituo  Kikuu  cha mabasi  mjini  Mbeya ,  wapiga  debe ,  mawakala  wa  mabasi  wakiwemo  na  baadhi ya  wafanyabiashara ndogo  kituoni  hapo   waliguswa na  kuhamasika  na   kufanya  harambee   katika   jitihada  kuhakikisha  anasafirishwa  hadi  mjini  Sumbawanga  ambako  angeweza kukutana  na  ndugu  zake  kutoka  kijijini  kwake Majimoto .

“ Sisi  kwa umoja  wetu  tuliguswa  sana  hiyo   tukatangaza  harambee  na kufanikiwa kukusanya   Sh.256,000 ambapo  tulitumia  kiasi  cha  fedha  hiyo   kumnunulia  godoro , shuka  mpya na  dishi  kwa ajili  ya kujisaidia haja ndogo” alisema  Joseph  Saibaba kiongozi  wa  wapiga  debe na kuongeza:

“Tumemkatia tiketi  ya   viti   vinne  katika   basi  hili la  Mbeya  Express, unajua kwa  siku  nne  tulikuwa naye hapa  stendi   tukimpatia huduma  zote   muhimu  ikiwemo  chakula  na  maji  kiasi   hiki  cha Sh.190,000 kilichosalia  tumemkabidhi  yeye ili   zimsaidie   huko  aendako”.

Mapengo alifanikiwa kusafirishwa na basi la Mbeya Express  T 844 ARZ  kutoka mjini  Mbeya  hadi Sumbawanga, baada  ya wasamaria  wema  kumkatia  tiketi  za viti   sita  nyuma   va  gari  hilo  ambapo  alilazwa katika viti hivyo.

Aidha kutokana ubovu wa barabara na gari hilo walilazimika kufika mjini hapa nyakati za saa 4 usiku ambapo baada ya kuwasili stendi kuu ya mabasi mjini Sumbawanga hakukuta ndugu yake yoyote aliyejitokeza kumlaki.

Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Rukwa, Peti Siyame alilazimika kuwasiliana na uongozi wa polisi Mkoa wa Rukwa ili uweze kutoa msaada kwa mtu huyo.

Kamanda  wa Polisi  wa Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda  alifika mara moja  kituoni  hapo  na  kuamuru basi  hilo alilosafiri  nalo  limfikishe  hadi  katika  Hospitali  ya Mkoa  wa Rukwa  mjini  Sumbawanga  ambapo  alipokelewa na  amelazwa kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, akizungumza hospitali hapo Mapengo anasisitiza kuwa anachotaka yeye ni kurudi nyumbani kwake majimoto umbali wa kilometa zaidi 180 kwa kuwa ugonjwa anaoumwa hawezi kupona na hana ndugu yoyote mjini Sumbawanga ambaye angeweza kumuhudumia sasa kulazwa hospitalini ni kuendelea kupata mateso.


Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa